Sunday, June 13, 2010

MNAMKUMBUKA HUYU MWENYE FULANA YA NJANO?















Huyu jamaa ni yule aliyejipatia umaarufu kwa kuingia uwanjani na kwenda kumkumbatia mchezaji wa kimataifa Ricardo Kaka wakati Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakicheza na timu ya Brazili katika mechi ya kirafiki iliyochezwa ndani ya uwanja wa taifa.

Jamaa alisema kwamba, tangu anatoka nyumbani alikuwa amepanga kufanya hivyo na kujiandaa kwa lolote litakalompata ili mradi tu lengo lake litimie.Wewe ungekuwa na ujasiri huo?


No comments:

Post a Comment