![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEharvOvb5igPW8utxcvIFiNaP9LV4rmYY0BNd7gi18W9bxzj4nXZjUDyOl4nljCVnS2csa4VvetPk1A4VfkK_RdQiAm_wdbaaGjo_TaBT5lgBFPAmjQJh8IOpKkBhV_Fu8W49orghRSNWHB/s320/shekoloa.jpg)
Anaitwa Sufiana Hassan Shekoloa, mzaliwa wa Kijiji cha Mlalo miaka hamsini na kitu iliyopita. Awali alikuwa ni Mkufunzi wa vyuo mbalimbali nhini kabla ya kuacha na kurudi nyumabani na kuwa mwalimu katika shule iliyokuwa chini ya KKKT ya Lwandai Sec School.
Mwanzo mwa miaka ya tisini akajiwa na wazo la kuanzisha shule iliyoitwa Mlalo Sekondary School ambayo mpaka ni mwalimu mkuu. Kiwango chake cha elimu ni Digrii ya ualimu aliyoipata katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
Mchango wake kwa watu wa Mlalo unatambulika na kwa muda mrefu amekuwa na shauku za kugombea ngazi mbalimbali za uongozi ili awatumikie wananchi na kuwaletea maendeleo. Akiwa ni kada wa CCM mwaka huu ameamua kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mlalo, lengo likiwa ni kumpokea kijiti cha uongozi kaka yake Brigedia Hassan Gwilizi.
Jamani tumpe sapoti, mshua wangu huyu namjua vizuri sana, ni mtu anayependa sana kutumikia watu, wanaomfahamu wanalijua hilo.
No comments:
Post a Comment